London,England.
Liverpool imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Chelsea katika mchezo wa mapema wa ligi kuu England uliopigwa mchana wa leo katika dimba la Stamford Bligde.
Chelsea ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao baada ya kiungo Ramirez kufunga kwa kichwa dakika ya 4 akiunganisha krosi safi ya mlinzi wa kushoto Cesar Azpilicueta.
Baada ya kuingia kwa bao hilo Liverpool iliamka na kuanza kulisakama lango la Chelsea na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika ya 45 kupitia kwa kiungo wake wa pembeni Philipe Coutinho.
Dakika ya 74 Liverpool ilipata bao la pili kupitia kwa Philipe Coutinho tena kisha mshambuliaji Christian Benteke akaongeza bao la tatu dakika ya 82 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Chelsea na kufunga kirahisi.
Kufuatia kipigo hicho Chelsea inabaki na pointi zake 11 ikiwa katika nafasi ya 15 na kukiweka shakani kibarua cha kocha wake Jose Mourinho ambaye yuko katika hatihati ya kutimuliwa.
0 comments:
Post a Comment