Friday, October 16, 2015
Klabu ya soka ya Sunderland ya England mwishoni mwa wiki hii wataandika historia katika sekta ya michezo barani Afrika na hasa katika nchi ya Tanzania.
Klabu hiyo itafungua kituo cha hifadhi ya michezo kwa vijana wadogo kituo hicho kilipo eneo la kidongo chekundu Jijini Dar es saalam.
Kituo hicho kitatoa huduma za kimichezo, kielimu na afya kwa wanamichezo chipukizi wanaochipukia nchini Tanzania.
Timu ya Sunderland imeshirikana na kampuni ya kuzalisha umeme ya Marekani ya (Symbion Power) kutengeza sehemu hiyo ya michezo itayokua ikiitwa JMK Youth Park.
kirefu cha jina la kituo hicho ni JMK, ni jina la Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete.
Mkurugenzi wa Sunderland Margaret Byrne, ameiambia BBC wanatarajia kituo hicho cha michezo kitawasaidia wanamichezo wachanga wa kizazi cha sasa kuendeleza vipaji vyao.
Kituo hicho kina viwanja vitatu vya nyasi bandia, kiwanja kimoja cha mchanga, viwanja viwili vya mchezo wa mpira wa kikapu, huku kukiwa na taa kwenye viwanja hivyo kwa ajili ya michezo ya usiku.
Uzinduzi wa hifadhi hiyo ya michezo ni mpango ulipo kati klabu hii ambayo pia inafahamika kama Black Cats na bara la Afrika katika kufundisha makocha, wachezaji wadogo na kuzijengea uwezo timu za barani Afrika.
Mahusiano ya klabu hii na bara la Afrika yalianza mwaka 2012 walipopata udhamini wa kampuni ya mafuta ya Tullow.
Sehemu ya makubaliano ya mkataba huu ilikua ni kuitangaza Afrika ambapo jezi ziliandikwa "wekeza Afrika” na huu ndio utafauti wa kalabu hii na vilabu vingine vya ligi ya England vinavyowekeza katika nchi za China na Marekani.
Kuna watu zaidi ya milioni 200 kutoka ukanda wa jangwa la Sahara, wanafuatilia ligi kuu ya England.
Pamoja na kutokua timu maarufu sana barani humu lakini timu hii inaendeleza miradi ya kijamii katika nchi za Ghana, Zambia, Afrika Kusini na Tanzania kusaidia kufundisha mpira katika ngazi ya chini.
Related Posts
MVUTO WA MAPENZI HUMVUTA ALIYEMVALI
MVUTO WA MAPENZI, HUMVUTA ALIYEMBALI, RUDISHA MAHUSIANO YAKO NDANI YA ...
JIUNGE LEO NA CHAMA HURU CHA FREEMASON
UKWELI NA UWAZI KUHUSU FREEMASONUSIPIGE SIMU AU KUTUMA SMS HADI UWE UM...
BINGWA WA KUREJESHA MTU ALIYECHUKULIWA MSUKULE
Msukule ni mtu au sehemu ya ...
Man City kuanza ligi kwa kishindo
Manchester City wataanza kuwa wageni wa Chelsea katika wiki ya kwanza ...
RASMI:JOHN TERRY ATUA ASTON VILLA
Birmingham,England. KLABU ya Aston Villa inayoshiriki ligi ...
URENO BILA RONALDO YATWAA NAFASI YA TATU KOMBE LA MABARA
Moscow, Urusi. IKICHEZA bila ya staa na nahodha wake,Cristi...
MCHAKATO WA UCHAGUZI MKUU WA TFF WASITISHWA
Dar Es Salaam,Tanzania. KATIKA hali isiyotarajiwa mchakato ...
MANNY PACQUIAO KWISHA HABARI YAKE ADUNDWA NA MWALIMU WA SHULE YA MSINGI NA KUPOKONYWA MKANDA WA WBO
Brisbane,Australia. BONDIA wa Ufilipino,Manny Pacquiao amee...
PEPE APATA TIMU MPYA BAADA YA USAJILI WAKE KWENDA PSG KUBUMA
Istanbul,Uturuki. BEKI wa kimataifa wa Ureno, Képler Lavera...
TOTTENHAM YATAMBULISHA JEZI ZAKE MPYA BAADA YA KULAMBA DILI LA MAANA KUTOKA NIKE
London,England. TOTTENHAM imetambulisha rasmi jezi zake mpya...
- Blogger Comments
- Facebook Comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment