Rio de Janeiro,Brazil.
Mfalme wa soka duniani Edson Arantes do Nascimento (Pele) amemtaja Lionel Messi kuwa ndiye mchezaji bora zaidi duniani kuliko mpinzani wake wa muda mrefu Cristian Ronaldo.
Akijibu swali aliloulizwa na waandishi wa habari akiwa njiani kuelekea India kwa ajili ya masuala ya mpira,Pele (74) amesema kuwa Messi ndiye mchezaji bora wa miaka kumi iliyopita,bora katika kizazi cha sasa cha mpira.
"Ni vigumu kulinganisha wachezaji wa vizazi/zama tofauti.Lakini kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita Messi amekuwa bora zaidi.Ronaldo anajaribu kucheza mbele na kufunga magoli lakini Messi anacheza katika staili/namna ya peke yake.Ningependa kuwa nao wote katika kikosi changu bila kumsahau Neymar ambaye naye anakuja vizuri"
Akiulizwa pia kama angeweza kutamba katika zama hizi kama alivyotamba zama zake Pele alijibu "Hakuna shaka kuwa mpira kwa sasa umebadilika sana lakini kama Mungu amekupa zawadi (kipaji) utakuwa tu bora katika zama zote"
Kuhusu kugombea Urais FIFA,Pele ansema "Sina mpango wa kugombea nafasi yoyote ile FIFA"
0 comments:
Post a Comment