728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, October 11, 2015

    MLINZI JOHN STONES AIBUKIA BARCELONA,MPANGO MZIMA JANUARI

    Barcelona,Hispania.

    Majaariwa ya Chelsea kumsajili mlinzi wa Everton John Stones huenda yakagonga mwamba baada ya Barcelona kuripotiwa kuingia katika mbio za kumnasa nyota huyo wa kimataifa wa England.

    Taarifa kutoka katika gazeti la michezo la Catalunya (Barcelona) la Mundo Derpotivo limesema Barcelona imemuweka Stones kwenye orodha ya nyota itakaowasajili mwezi januari 2016 ili kuimarisha safu yake ya ulinzi inayolega lega baada ya Thomas Vermalen,Jeremy Mathieu na Marc Bartra kushindwa kuonyesha makali yao kutokana na sababu mbalimbali.

    Mbali ya Stones,21 Mundo Derpotivo linazidi kupasha kuwa Barcelona pia imewaorodhesha walinzi Jose Gimenez (Atletico Madrid), Marquinhos (Paris Saint-Germain) na Aymeric Laporte (Athletic Bilbao) na tayari uongozi wa juu wa mabingwa hao wa Ulaya umejipanga kufanya kweli punde tu ifikapo mwezi januari 2016.




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MLINZI JOHN STONES AIBUKIA BARCELONA,MPANGO MZIMA JANUARI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top