728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, October 12, 2015

    ARSENAL KUIMARISHA KIUNGO CHAKE MWEZI JANUARI KWA KUMSAJILI MUISRAELI

    London,England.

    Kutoka gazeti la Evening Times habari zinasema Arsenal inajiandaa kutuma ofa Celtic kwa ajili ya kumsajili kiungo mkabaji Nir Bitton.

    Evening Times linazidi kupasha kuwa mapema wiki iliyopita Arsenal ilituma maskauti wake kwenda kumtazama kiungo huyo wakati akiichezea Celtic dhidi ya Fenerbahce katika mchezo wa Europa Ligi ulioisha kwa sare ya goli 2-2.

    Arsenal inahangaika kutafuta kiungo mpya mkabaji atayekuja kuja kusaidiana na Francis Coquelin baada ya viungo Mathieu Flamini na Mikel Arteta kushindwa kuonyesha kiwango kizuri kutokana na majeraha ama umri kuwatupa mkono.

    Mbali ya Arsenal,Bitton pia ameripotiwa kufukuziwa na vilabu vingi vya ligi kuu England kutokana na kuendelea kuonyesha kiwango kikubwa.

    Bitton alijiunga na Celtic mwaka 2013 kwa ada ya £700,000 akitokea klabu ya FC Ashdod ya nyumbani kwao Israeli na kufanikiwa kutwaa mataji mawili ya ligi ya Scotland.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ARSENAL KUIMARISHA KIUNGO CHAKE MWEZI JANUARI KWA KUMSAJILI MUISRAELI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top