728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, October 22, 2015

    VPL:AZAM FC BADO YAIFUKUZA YANGA,YAICHAPA NDANDA FC KWAO,MWADUI MOTO,MBEYA CITY SAFI,MTIBWA SUGAR YABANWA

    Ligi kuu Tanzania bara (VPL) imeendelea tena leo jioni kwa michezo minne kupigwa katika viwanja mbali mbali hapa nchini.

    Katika mchezo uliopigwa huko Mtwara katika dimba la Nangwanda Sijaona,wenyeji Ndanda FC wamekubali kichapo cha goli 1-0 toka kwa Azam FC.Goli pekee la mchezo huo limefungwa na mlinzi Shomari Kapombe

    Kufuatia ushindi huo Azam FC imefikisha pointi 19 ikiwa sawa na Yanga iliyo kileleni kutokana na wingi wa magoli ya kufunga.

    Katika michezo mingine JKT Ruvu imeibana Mtibwa Sugar na kutoka nayo sare tasa ya 0-0 katika mchezo mkali ulipoigwa huko Mabatini.

    Shinyanga:Kutoka Shinyanga,Mwadui FC imeibuka na ushindi mnono baada ya kuibamiza Mgambo FC kwa magoli 3-0 katika mchezo uliopigwa huko Mwadui.Magoli ya Mwadui yamefungwa na Jerryson Tegete aliyefunga mara mbili pamoja na Malika Ndeule.

    Mbeya:Mbeya City imetoka kifua mbele katika dimba la Sokoine baada ya kuibamiza African Sports kwa jumla ya bao 1-0.Goli la Mbeya City limefungwa na Geofrey Mlawa.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: VPL:AZAM FC BADO YAIFUKUZA YANGA,YAICHAPA NDANDA FC KWAO,MWADUI MOTO,MBEYA CITY SAFI,MTIBWA SUGAR YABANWA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top