Kama mambo yasingeenda ndiyo sivyo leo hii straika kinda Antony Martial angekuwa ni mchezaji wa Chelsea akinolewa na Mreno Jose Mourinho badala ya Mdachi Louis Van Gaal.
Kutoka gazeti la Ufaransa liitwalo CanalPlus habari zinasema Chelsea ilitaka kumsajili Martial,19 msimu huu tena kwa dau zaidi ya lile la £36m ambalo Manchester United wamelitoa lakini straika huyo wa zamani wa AS Monaco akakataa katakata.
Sababu za Martial kukataa kujiunga na Chelsea ni kuwa nyota huyo ambaye mpaka sasa ameifungia Manchester United magoli manne katika michezo saba ni kuwa Manchester United ndiyo klabu ya ndoto zake hivyo kujiunga na miamba hiyo ya jiji la Manchester ni kutimiza ndoto hiyo ya muda mrefu.
Pia Martial ana amini Manchester United ni moja kati ya vilabu vikubwa vitano duniani na Chelsea haimo katika kundi hilo
0 comments:
Post a Comment