LONDON,ENGLAND.
Arsenal imelimwa faini ya paundi 60,000 ($92,052) na kupewa onyo kali kwa soka la kukiuka kanuni za uwakala baada ya kufanya biashara na mawakala kanjanja/wasio na sifa wakati ikimsajili mlinzi Calum Chambers toka Southampton julai 2014.
Taarifa kutoka FA zinasema Arsenal imepigwa faini hiyo kutokana na kumuhusisha wakala kanjanja Alan Middleton na wakala asiye na kibali (leseni) Philip Ercolano katika usajili huo ambao vilabu vya Arsenal na Southampton havikutaja bei ya mlinzi huyo lakini vyombo vya habari vikaripoti kuwa ni kati ya paundi milioni 11 mpaka 15.
FA imeongeza kuwa licha ya Arsenal kukiri na kukana baadhi ya makosa na kudai kuwa haikujua kama wakala Middleton hakuwa na vigezo/sifa za kumuwakilisha Chambers imesisitiza adhabu hiyo ni halali.
Wakala Alan Middleton yeye amelimwa faini ya paundi 30,000 huku pia akifungiwa kutokujihusisha na masuala ya uwakala wa wachezaji kwa kipindi cha miezi mitatu.
0 comments:
Post a Comment