Mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema ameibuka na kauli iliyotafsiriwa kuwa ni kuiponda Arsenal baada ya kudai kuwa habari za yeye kutaka kutua katika klabu hiyo zilimfanya acheke kupindukia.
Akifanya mahojiano na jarida la Journal du Dimanche la Ufaransa,Benzema,27 amesema alicheka sana yeye na kaka yake kuhusiana na uvumi huo na kusisitiza kuwa hana mpango wa kuhama Real Madrid.
Amesema "Kama ilivyo kawaida katika majira yote ya joto,huwa nacheka nikiwa na kaka yangu na rafiki zangu.Tunasubiri vyombo vya habari vije na habari hizi,tucheke.
"Real na Barca ndiyo kilele cha soka duniani sasa kwanini nihame??Niko kikosi cha kwanza katika klabu bora zaidi duniani.Nina furaha hapa,ni hayo tu.Alimaliza Benzema.
0 comments:
Post a Comment