Timu ya taifa ya Ureno imemaliza michezo yake ya kusaka tiketi ya kucheza michuano ijayo ya Ulaya (Euro 2016) kwa kupata ushindi wa magoli 2-1 ugenini mbele ya timu ya taifa ya Serbia.
Ureno ambayo tayari ilikuwa imeshafuzu hata kabla ya mchezo huo huku ikiwa imewapumzisha nyota wake kibao ilijipatia goli la kuongoza dakika ya 5 tu ya mchezo kupitia kwa nahodha wake Luis Nani kabla ya kupata la pili dakika ya 68 kupitia kwa kiungo Joao Moutinho.
Serbia ambayo ilipata pigo kwa nyota wake wawili kulimwa kadi nyekundu Nemanja Matic na Alexander Kolalov baada kuonyesha mchezo usiokuwa wa kiungwana ilijipatia goli la kufutia machozi dakika ya 65 kupitia kwa Zoran
Tosic.
Kufuatia ushindi huo Ureno imefikisha pointi 21 ikiwa na pointi 7 zaidi ya Albania iliyo katika nafasi ya pili ambayo nayo imefuzu toka katika kundi hilo baada ya kuifunga Armenia kwa jumla ya magoli 3-0.
Vikosi
Serbia: Stojkovic, Tomovic, Stefan Mitrovic,Dusko Tosic, Kolarov (Obradovic 77), Zoran Tosic (Sulejmani 85), Milivojevic, Ljajic,Matic, Tadic, Aleksandar Mitrovic (Skuletic
85)
Portugal: Rui Patricio, Semedo, Fonte, Bruno Alves (Neto 46), Eliseu, Nani, Andre Andre,Danilo Pereira, Veloso, Quaresma, Danny (Eder 57).
0 comments:
Post a Comment