Madrid,Hispania.
Gazeti la michezo la Don Balon la Hispania limekuja na habari ambayo siyo nzuri sana kwa mashabiki wa Arsenal duniani kote.
Don Balon limeripoti kuwa Real Madrid inaandaa kitita cha £37.3m pamoja na winga Denis Cheryshev ili kumsajili staa wa Arsenal Mchile Alexis Sanchez (26) aliyewahi pia kukipiga na FC Barcelona.
Real Madrid imeamua kumjumuisha Cheryshev mwenye thamani ya £15m katika dili hilo kutokana na winga huyo raia wa Urusi kuwa ni kipenzi kikubwa cha kocha wa Arsenal Mfaransa Arsene Wenger.
0 comments:
Post a Comment