728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, October 27, 2015

    KOCHA MZUNGU WA TOTO ABWAGA MANYANGA,KERO ZA WACHEZAJI ZADAIWA KUCHANGIA

    Mwanza,Tanzania.


    Kocha mkuu wa Toto Africans, Martin Grelics ameachia ngazi kuifundisha miamba hiyo ya jiji la Mwanza kutokana na kuchoshwa na hali ya mambo inavyoenda ndani ya klabu.

    Grelics aliyeinoa timu hiyo kwa takriban miezi miwili tangu alipotua nchini,ameiongoza timu hiyo kucheza mechi nane mpaka sasa za Ligi Kuu, ikishinda mbili, kutoa sare mara nne huku ikifungwa mara mbili.
    Kwa mujibu wa barua ya Oktoba 23, ambayo Grelics ameuandikia uongozi wa Toto, matatizo yaliyosababisha abwage manyanga ni yale yanayotokana na sababu za nje ya uwanja na si vinginevyo.

    “Nimeamua kuchukua uamuzi huu kutokana na matukio kadhaa yaliyojitokeza wiki chache zilizopita. Uamuzi huu wa kujiuzulu hautokani matokeo ya mechi tulizocheza au dhidi ya wachezaji. Ninafurahia kuwa nao kila mara mazoezini pamoja na kwenye mechi. Kutokana na sintofahamu iliyojitokeza hivi karibuni, tuliweza kuwa na programu ya mazoezi kwa siku saba mwezi uliopita.

    Hali kama hiyo haikubaliki kwa timu na kocha anayezingatia weledi kama mimi. Nimelazimika mara nyingi kubeba majukumu ya ndani ambayo yalitakiwa kusimamiwa na uongozi. Wachezaji kutolipwa mishahara, safari ya hatari kule Tanga na Tabora, wachezaji kuishi kwenye mazingira magumu na uongozi kutoonyesha maendeleo yoyote.

     “Nimeamua kuchukua uamuzi wa kujiuzulu. Nadhani uamuzi wangu utasaidia uongozi kubadilika na kuifanya timu ifanye vizuri kwenye ligi. Naamini Toto ina wachezaji wazuri wanaoweza kuifanya timu ibaki kwenye Ligi Kuu,” ilisema barua hiyo.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KOCHA MZUNGU WA TOTO ABWAGA MANYANGA,KERO ZA WACHEZAJI ZADAIWA KUCHANGIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top