728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, October 13, 2015

    EVRA AMTAJA ATAKAYEIBEBA UFARANSA EURO 2016,AMTAMANI RIBERY

    Paris,Ufaransa.


    Mlinzi wa Ufaransa Patrice Evra amesema Karim Benzema ataipa mafanikio timu hiyo katika fainali zijazo za Ulaya zitakazopigwa 2016 huko Ufaransa.

    Akiongea hivi  na RMC,Evra amesema ana imani kubwa juu ya uwezo wa Benzema kwani ni mchezaji mzuri sana waliyenae katika kikosi cha sasa hivyo hana wasiwasi juu ya kutwaa ubingwa huo.

    Anasema "Kwangu,Karim ni mchezaji mzuri sana nadhani hata machoni mwa kocha Didier Deschamps ndivyo ilivyo.Anapaswa kupuuza wanaombeza na kuongeza bidii uwanjani.Nimemwambia aendelee kujifua na anajua kuwa tupo kwa ajili ya kuhakikisha anafanya vizuri katika michuano hiyo.Wachezaji kama Karim wana majukumu makubwa.Tukiwa nae tunaweza kutwaa Euro.

    Akiongea kuhusu Ribery,Evra amesema "Kati ya vitu ninavyovitamani ni kumuona tena Frank Ribery akirudi kikosini.Ni mtu mzuri sana.Kama ataamua kurudi tena kikosini ,nitamkaribisha kwa mikono miwili.Lakini mimi siyo kocha,hilo liko mikononi mwa kocha.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: EVRA AMTAJA ATAKAYEIBEBA UFARANSA EURO 2016,AMTAMANI RIBERY Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top