London,England.
Chelsea imeendelea kuwa na wakati mguu msimu huu baada ya kuamuriwa na chama cha soka nchini England (FA) kulipa faini ya paundi 25,000 baada ya wachezaji wake watano kulimwa kadi za njano katika mchezo wa jumamosi iliyopita dhidi ya Westham na Chelsea kulala kwa goli 2-1.
Kwa mujibu wa sheria za FA klabu yoyote ambayo wachezaji wake watano au zaidi wataonyeshwa kadi za njano katika mchezo mmoja itatafsiriwa kuwa imeshindwa kudhibiti nidhamu na italimwa faini.
Katika mchezo wa jumamosi wachezaji Cesar Azpilicueta, Willian,Cesc Fabregas, John Obi Mikel Diego Costa na Nemanja Matic walilimwa kadi za njano baada ya kufanya makosa mbalimbali.Baadae Matic alilimwa kadi nyekundu.
Taarifa zaidi zinasema kuwa faini hiyo haitahusiana la tukio la mwamuzi John Moss kuwatoa uwanjani kocha Jose Mourinho na msadizi Silvino Louro lakini huenda Mourinho akajikuta matatani baada ya kukataa kufanya mahojiano na vyombo vya habari baada ya mchezo wa huo.FA hutoa adhabu kwa kocha anayekataa kufanya mahojiano na vyombo vya habari baada ya mchezo.
0 comments:
Post a Comment