Colorado,Marekani.
Mshambuliaji Didier Drogba ameendelea kuonyesha kuwa bado wamo baada ya hapo jana jumamosi kuifungia goli klabu yake ya Montreal Impact katika ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Colorado Rapids katika mchezo wa kuwania tiketi ya kuingia katika hatua ya sita bora ya kanda ya mashariki (Eastern Conference) ya michuano ya ligi ya Marekani MLS.
Drogba,37 alifunga goli hilo dakika ya 15 baada ya mpira wake wa faulo (free kick) wa umbali wa mita 30 kumshinda kipa wa Colorado Rapids Zac MacMath na kujaa wavuni na kuisogeza Montreal Impact katika nafasi ya sita ikiwa imejikusanyia alama 40.
Faulo hiyo ilitolewa baada ya kiungo wa Rapids Dillon Powers kumchezea vibaya kiungo wa Montreal Impacts Andres Romero.
Kufuatia goli hilo mpaka sasa Drogba anakuwa ameifungia Montreal Impact magoli tisa katika michezo tisa tangu ajiunge nayo msimu huu akitokea Chelsea.
0 comments:
Post a Comment