Kiungo Mbrazili wa Yanga, Andrey Coutinho amemuomba kocha wake, Hans van Der Pluijm ampe dakika 45 tu ili aisambaratishe Azam kesho katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa.
Tangu msimu huu uanze Septemba 12, Coutinho amekuwa na maisha magumu kutokana na kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza lakini ameomba dakika hizo na anaamini atafanya kweli.
“Ninafanya mazoezi magumu kuhakikisha nakuwa fiti ili nipate nafasi ya kucheza, najua kazi ni kubwa, namuomba kocha anipe nafasi japo kwa dakika 45 zinanitosha kabisa kumuonyesha uwezo wangu,” alisema Coutinho ambaye mkataba wake na Yanga unamalizika mwishoni mwa msimu huu.
Coutinho amekuwa anatulia benchi katika mechi zote tano za mwanzo ambazo Yanga imecheza.
Msimu huu haujawa mzuri kwake kwa kuwa hajaweza kumshawishi kocha Hans van der Pluijm kutoka Uholanzi.
(Salehjembe.com)
0 comments:
Post a Comment