Santiago,Chile.
Staa wa Chile na Arsenal Alexis Sanchez amesema kuwa havutiwi kabisa na habari zilizoenea kuwa Real Madrid inataka kumsajili hapo mwakani (2016) na kusisitiza kuwa anaipenda Arsenal,wachezaji wenzake na jiji la London na kuwa hana mpango wa kurudi Hispania.
Akiongea kutoka Chile alikokuwa akiitumikia timu yake ya taifa ya Chile katika michuano ya kusaka tiketi ya kombe la dunia la mwaka 2018 huko Urusi amesema
"Sifahamu chochote kile ambacho kinasemwa na vyombo vya habari,najisikia furaha kuwa Arsenal.Ninafuraha pamoja na wachezaji wenzangu,nalipenda jiji la London na sitaweza kubadilika,nina furaha.Bado nitabaki hapa kwa kipindi kirefu"Alimaliza Sanchez na kuongeza kuwa mama yake ni kama kocha kwake kwani humpigia simu mara kwa mara na kumsisitiza kuwa awe anapiga mashuti mara kwa mara ili kufunga magoli mengi na ndicho anachokifanya.

0 comments:
Post a Comment