Liverpool imepata pigo baada ya mlinzi wake wa kushoto Joe Gomez kupata jeraha la goti litakalomuweka nje ya uwanja kwa kipindi cha kati ya miezi 8 mpaka 9.
Gomez,18 ambaye amejiunga na Liverpool msimu huu akitokea klabu ya daraja la kwanza ya Charlton Athletic kwa ada ya awali ya £3.5m alipata jeraha hilo jumanne usiku wakati akiichezea timu ya U-21 ya England iliyokuwa ikimenyana na Kazakhstan huko Coventry City.
Gomez ameichezea Liverpool michezo sita ya ligi kuu huku pia akifanikiwa kucheza michezo miwili ya Europa dhidi ya Bordeaux na FC
Sion.
0 comments:
Post a Comment