Munich,Ujerumani.
Mshambuliaji aliye katika kiwango cha hatari msimu huu Mpoland Robert Lewandowski amefichua siri na kuweka bayana kile kinachofanya awe akifunga magoli kila kukicha.
Lewandowski ambaye mpaka sasa amefunga jumla ya magoli 24 akiwa na Bayern Munich na timu ya taifa ya Poland amesema ukali wake unatokana na mazoezi maalumu yanayotolewa na makocha wa Bayern Munich.
Akiongea na jarida la Shortlist,Lewandowski amesema "Bayern kuna mazoezi maalumu kwa ajili ya washambuliaji pekee ambayo nimekuwa nikijitahidi sana kuyamudu.Unapoona magoli yanaingia,unatamani yaendelee kuingia mara kwa mara na hiyo inamaanisha kuwa unapaswa kuongeza bidii.Unachokifanya mazoezini kitajionyesha kwenye mechi"
"Watu wamekuwa wakiniuliza kama hiki ndicho kilele cha kiwango changu,labda lakini naamini naweza kuwa mkali zaidi ya hapo.Naamini hilo.
0 comments:
Post a Comment