Dar es salaam,Tanzania.
Licha ya mshambuliaji Donald Ngoma kukosa penati katika kipindi cha kwanza,Yanga imeendelea kuonyesha makali yake baada ya jioni ya leo kuibuka na ushindi mnono wa goli 4-1 dhidi ya Toto Africans katika mchezo mkali wa ligi kuu Tanzania bara uliopigwa katika uwanja wa taifa,Dar es salaam.
Yanga ilipata goli lake la kwanza dakika ya (9') kupitia kwa mlinzi wake Juma Abdul aliyefunga kwa shuti kali la mita 20 akiunganisha kona fupi ya kiungo Haruna Niyonzima.Goli la pili limefungwa na Simon Msuva (49') huku Hamis Tambwe akifunga la tatu dakika ya ( 81') kisha Msuva kufunga goli la nne dakika ya (90') akiunganisha krosi ya Andrey Coutinho huku goli la kufutia machozi la Toto likifungwa dakika ya (62') na Miraji Athumani.
Kufuatia ushindi huo Yanga imefikisha jumla ya pointi 19 na kuendelea kujikita kileleni baada ya kucheza michezo 7 ikizidi Azam iliyo nafasi ya pili kwa pointi 3.Azam itashuka dimbani kesho siku ya alhamisi kuvaana na Ndanda huko Mtwara.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul/Simon Msuva dk46, Mwinyi Mngwali, Kevin Yondan/Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Vincent Bossou, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma, Amissi Tambwe, Malimi Busungu na Godfrey Mwashiuya/Andrey Coutinho.
Toto Africans; Mussa Mohammed, Hassan Khatib, Robert Magadula/Miraj Makka, Hamisi Kasanga, Carlos Protas, Salimn Hoza/William Kimanzi, Japhet Vedastus/Jaffar Mohammed, Abdallah Seseme, Evarigetus Bernad, Edward Christopher na Miraji Athumani.
Matokeo mengine
Prisons 1-0 Simba SC
Coastal Union 1-0 Kagera Sugar.
Stand United 3-0 Majimaji
0 comments:
Post a Comment