Na Paul Manjale
Ospina:Mlinda mlango wa Arsenal David Ospina ameripotiwa kuwa atafikiria kuachana na klabu hiyo ikiwa atawekwa benchi katika mchezo wa jumanne wa ligi ya mabingwa dhidi ya Bayern Munich na nafasi yake kuchukuliwa na mlinda mlango Peter Cech.(The People)
Alcacer:Kocha wa Chelsea Mreno Jose Mourinho anataka kukiongezea makali kikosi chake ifikapo mwezi januari kwa kumsajili mshambuliaji wa Valencia Paco Alcacer.Alcacer,22 anaweza kuhama Valencia ikiwa Chelsea itakuwa tayari kutoa kitita cha £50m.(The Sun)
Kokorin:Klabu ya Arsenal imeendelea kuonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Dynamo Moscow Alexander Kokorin baada ya kuripotiwa kuandaa kitita cha £7m ili kumleta Emirates mkali huyo wa mabao hapo mwezi januari mwakani.Arsenal inaona dau hilo ni sahihi kwani nyota huyo amebakisha muda mfupi katika mkataba wake unaofikia ukingoni mwezi juni.(The Sun)
Montoya:Kocha wa Liverpool Mjerumani Jurgen Klopp ameitaka klabu hiyo kuachana na mpango wa kutaka kumsajili mlinzi wa kulia wa Barcelona,Martin
Montoya na badala yake ielekeze nguvu zake katika kumnasa kiungo wa Juventus Claudio Marchisio mwenye thamani ya £23.5m.(Sunday Mirror )
Austin:Mshambuliaji wa QPR Charlie Austin anajipanga kuzikataa ofa zote zitakazoletwa na vilabu vya ligi kuu hapo mwezi januari ili aweze kuondoka QPR akiwa mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu.(Sunday Mirror)
Moyes:Kocha David Moyes yuko tayari kuachana na Real Sociedad ili kuchukua kibarua ya kuinoa Aston
Villa kama nafasi hiyo itapatikana baada ya kuwepo kwa habari kuwa klabu hiyo ya jiji la Birmingham iko mbioni kumfuta kazi kocha wake wa sasa Tim Shearwood.(The Daily star Sunday)
Gohi:Klabu ya West Ham imeripotiwa kumfukuzia kwa karibu mshambuliaji wa Oostende Muivory Coast Gohi Bi Zoro Cyriac ili kuongeza nguvu katika kikosi chake kinachopambana kumaliza katika nafasi za juu katika ligi kuu ya England.(The Daily star Sunday)
0 comments:
Post a Comment