Manchester United imeripotiwa kuwa katika mawindo makali kwa ajili ya kumsajili kiungo kinda wa Serbia Marko Grujic,hii ni kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail.
Inasemekana Manchester United ilituma maafisa wake kwenda kumtazama kiungo huyo wakati akiichezea klabu yake ya Red Star Belgrade dhidi ya FK Rad Beograd wikendi iliyopita.Grujic anawindwa ili kuja kuziba nafasi za viungo Michael Carrick na Baster Schweinsteiger ambao umri unazidi kuwatupa mkono.
Katika mchezo huo Grujic, 19, mwenye urefu wa futi 6.3 na ambaye kiuchezaji anafananishwa na kiungo wa Chelsea Nemanja Matic,alifunga goli moja katika ushindi wa magoli 3-0 iliyoupata Red Star Belgrade dhidi ya FK Rad Beograd.Res Star inamuuza kiungo huyo kwa paundi 3milioni
Mbali ya Manchester United,Chelsea nayo imeripotiwa kuwa katika mawindo ya kumsaka Grujic, ambaye alikuwa ni tegemeo katika kikosi cha vijana cha Serbia cha U20 kilichotwaa kombe la dunia mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment