Dar es Salaam,Tanzania.
Makocha na wachambuzi
wa soka nchini wamemtaka kocha wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Charles Mkwassa kuwafundisha kumiliki
mpira wachezaji wake kabla ya mchezo wa mwezi ujao dhidi ya Algeria.
Taifa Stars imefuzu kwa hatua ya pili ya kusaka kucheza Kombe la Dunia 2018,baada ya kuifunga Malawi kwa ushindi jumla wa mabao 2-1.
Katika mchezo uliofanyika Malawi jumapili,Stars ilizidiwa kwa sehemu kubwa na Malawi hasa katikati ya uwanja hali iliyochangia kipigo cha bao 1-0, lakini
ushindi wa kwanza wa mabao 2-0 uliisaidia Tanzania kufuzu.
Wachambuzi hao walifafanua kuwa Stars ilionyesha uwezo mdogo wa kumiliki mpira, kupoteza mpira kirahisi na
kutomuendea adui haraka baada ya kunyang’anywa mpira (kukabia macho).
“Hii ni kasoro ambayo kocha Mkwassa anapaswa kuifanyia kazi kabla ya
kuikabili Algeria timu yenye sifa kuu tatu katika soka, pia ina uwezo zaidi ya Tanzania na hata Malawi,” alisema
Mshindo Msolla aliyewahi kuwa kocha wa Stars miaka ya nyuma.
Msolla alizitaja sifa za Algeria kuwa ni timu yenye kasi, ina uwezo wa kumiliki mpira kwa ustadi na ina nguvu. “Tofauti
na sisi sifa hizo bado hatuna, ukiangalia kwenye mchezo wa Jumapili, mipira yote
ya kugombea waliichukua Malawi, hii ni kasoro ambayo inapaswa kufanyiwa kazi,alisema Msolla.
Mchezaji wa zamani wa Tanzania,Kitwana Manara alisema Stars haikuonyesha soka kama ilivyomenyana
na Nigeria katika mchezo wa kufuzu Afcon.
“Kwenye mechi ya juzi,katikati Stars ilipwaya, Malawi ilicheza kwa mtindo wa kutompa nafasi mpinzani, tunachopaswa ni kujipanga, mechi ijayo ni ngumu zaidi.
“Algeria walifika hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia hivyo ina uzoefu, TFF inatakiwa kuiandaa timu mapema na
kupata mechi nyingi za kimataifa za kujipima nguvu tena zisichezwe hapa
nyumbani,” alisema Manara
0 comments:
Post a Comment