728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, October 21, 2015

    LIGI KUU BARA:YANGA IKO NA TOTO,AZAM IKO MTWARA,RATIBA YA MICHEZO YA LEO/KESHO IKO HAPA

    Ligi kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) inatarajiwa kuendelea leo Jumatano kwa michezo minne kuchezwa katika viwanja tofauti nchini, huku timu 8 zikisaka kupata pointi tatu muhimu.

    Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Young Africans watawakaribisha Toto Africans,mchezo utakaonza majira ya saa 10:30 jioni,
    mjini Shinyanga Stand United watakua wenyeji wa Majimaji katika uwanja wa Kambarage
    mjini humo.

    Tanzania Prisons watawakaribisha Simba SC
    katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, huku Wagosi wa Kaya, Coastal Union wakiwakaribisha Kagera Sugar katika uwanja
    wa Mkwakani jijini Tanga.

    Alhamis ligi hiyo itanendelea kwa michezo minne pia kucheza katika viwanja mbalimbali,JKT Ruvu wataikaribisha Mtibwa Sugar uwanaj wa Karume jijini Dar es salaam,Mwadui FC watacheza dhidi ya Mgambo Shooting katika uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga.

    Jijini Mbeya, Mbeya City watawakaribisha African Sports katika uwanja wa Sokoine, huku Ndanda FC wakiwa wenyeji wa waoka mikate wa bakhresa Azam FC katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: LIGI KUU BARA:YANGA IKO NA TOTO,AZAM IKO MTWARA,RATIBA YA MICHEZO YA LEO/KESHO IKO HAPA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top