728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, October 28, 2015

    LIGI KUU BARA:YANGA USO KWA USO NA MWADUI SHINYANGA,SIMBA IKO TAIFA KUIVAA COASTAL UNION,KESHO AZAM MIKONONI MWA JKT RUVU,RATIBA YOTE IKO HAPA


    Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kuendelea kesho kwa michezo sita kuchezwa katika viwanja mbalimbali, ikiwa inaingia katika raundi ya tisa huku kila timu ikisaka ushindi wa pointi tatu muhimu.

    Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Simba SC watawakaribisha Coastal Union kutoka jijini Tanga, mchezo utakaonza majira ya saa 10:30 jioni, huku Ndanda FC wakiwa wenyeji wa Stand United uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

    Wachimba Almasi wa Mwadui FC watawakaribisha Yanga SC katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Toto African watakua wenyeji wa maafande wa Mgambo Shooting katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

    Wakata miwa wa Turiani, Mtibwa Sugar watakua wenyeji wa Kagera Sugar katika uwanja wa Manungu Complex mkoani Morogoro, huku watoza ushuru wa jiji la Mbeya katika uwanja wa Sokoine Mbeya City watakua wenyeji wa Majimaji kutoka mkoani Ruvuma.

    Ligi hiyo itaendelea siku ya Alhamis kwa michezo miwili kuchezwa, Tanzania Prisons watakua wenyeji wa African Sports katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, JKT Ruvu watakua wenyeji wa Azam FC katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: LIGI KUU BARA:YANGA USO KWA USO NA MWADUI SHINYANGA,SIMBA IKO TAIFA KUIVAA COASTAL UNION,KESHO AZAM MIKONONI MWA JKT RUVU,RATIBA YOTE IKO HAPA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top