KOCHA Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi, amesema wachezaji wake walikosa umakini dakika 10 za mwisho na kuruhusu bao la kusawazisha kwa timu ya Mwadui ya Shinyanga.
Yanga ikiwa mbele kwa mabao mawili yaliyofungwa na Donald Ngoma, safu yake ya ulinzi chini ya Nahodha wake, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ilishindwa kulinda ushindi wa timu hiyo na kujikuta ikifungwa bao lakusawazisha katika dakika za mwisho za mechi hiyo.
Akizungumza na BINGWA, Mwambusi alisema wachezaji wake walikosa umakini dakika za lala salama, wakaruhusu washambuliaji wa Mwadui kumsogelea kipa Ali Mustapha ‘Barthez’, hatimaye wakasawazisha bao hilo.
“Soka ni dakika 90, tulishawakamata Mwadui, lakini bahati mbaya vijana wakajisahau na wapinzani wakasawazisha bao katika dakika za mwisho kabisa za mchezo,” alisema Mwambusi.
0 comments:
Post a Comment