728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, October 15, 2015

    KUELEKEA MCHEZO DHIDI YA MBEYA CITY JUMAMOSI,KOCHA SIMBA ATOA SOMO KWA WACHEZAJI WAKE

    Dar es salaam,Tanzania.

    Dar es Salaam. Kocha wa Simba, Dyran Kerr amewataka wachezaji wake kutumia uzoefu wao kumudu mazingira ya Uwanja wa Sokoine ili kuibuka na ushindi dhidi ya Mbeya City,Jumamosi hii.

    Kerr amesema kuwa anazo
    taarifa juu ya ubovu wa sehemu ya kuchezea ya Uwanja wa Sokoine, lakini
    ana imani kubwa wachezaji wake watahimili mazingira hayo na kupata ushindi kwenye mchezo huo.

    Alisema kuwa mazingira ya viwanja vingi hapa nchini si mazuri ila hiyo haiwezi kuwa sababu ya kuizuia timu kupata ushindi na badala yake wachezaji wanatakiwa kutumia uwezo binafsi ili
    kuiwezesha timu kupata ushindi.

    “Sina hofu yoyote kuwa uwanja unaweza kutuzuia tusipate ushindi dhidi ya
    wapinzani wetu. Wachezaji wangu wako vizuri na nina uhakika watatumia uzoefu
    wao ili tushinde mechi hiyo.

    Pia nimesikia wanapenda kutumia mfumo wa mipira mirefu, kikubwa sisi hatuwezi
    kuwaiga bali tutacheza soka letu la siku zote,” alisema Kerr.Kerr aliongeza kuwa hatishwi na rekodi nzuri ya Mbeya City dhidi ya Simba na
    safari hii timu yake itavunja mwiko kwa kuibuka na ushindi.

    Alisema Simba itaingia uwanjani ikiiheshimu Mbeya City kama moja ya timu ngumu na bora nchini, lakini suala la ushindi kwenye mchezo huo liko pale pale.

    “Rekodi hazichezi na nadhani
    tumeshalithibitisha hilo kwa kushinda mechi mbili za kwanza kule Tanga ambako niliambiwa kuwa ni kugumu
    kupata ushindi. Wachezaji wangu wako tayari na tutaibuka na ushindi kwenye
    mechi hiyo,” alisema Kerr.

    Simba haijawahi kupata ushindi wa aina yoyote dhidi ya Mbeya City tangu timu
    hiyo ilipopanda daraja misimu miwili iliyopita, ambapo imeambulia sare mbili na vipigo viwili katika mechi nne iliyokutana na timu hiyo ya Mbeya.

    Timu hizo zilikutana kwa mara ya kwanza msimu wa 2013/2014 na zilitoka sare ya 2-2 kwenye Uwanja wa Taifa na Mbeya zilitoka 1-1.Katika msimu uliopita, Mbeya City
    ilichomoza na ushindi wa mabao 2-1 Dar es Salaam na Mbeya ilishinda 2-0

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KUELEKEA MCHEZO DHIDI YA MBEYA CITY JUMAMOSI,KOCHA SIMBA ATOA SOMO KWA WACHEZAJI WAKE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top