728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, October 23, 2015

    BAYERN KUWEKA REKODI YA AINA YAKE BUNDESLIGA WIKIENDI HII

    Munich,Ujerumani.

    Bayern Munich huenda ikaweka rekodi ya kushinda michezo 1000 ya ligi ya Bundesliga hapo kesho jumanosi iwapo itaifunga FC Cologne.

    Bayern Munich ambayo jumamosi iliyopita ilishinda mchezo wake wa 999 baada ya kuifunga Werder Bremen kwa bao 1-0 kesho itakuwa katika dimba lake la Allianz Arena ikiwa tayari imeshinda michezo tisa ya Bundesliga msimu huu hivyo ushindi dhidi ya FC Cologne utakuwa ni ushindi wake wa kumi.

    Ikiwa Bayern Munich itashinda mchezo huo wa jumamosi itakuwa imeweka rekodi ya kuwa klabu ya kwanza ya Bundesliga kushinda michezo 1000 katika michezo 1,713 ikifuatia na, Werder Bremen iliyoshinda michezo 740 katika michezo 1,739 tangu kuasisiwa kwa ligi ya Bundesliga mwaka 1963.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BAYERN KUWEKA REKODI YA AINA YAKE BUNDESLIGA WIKIENDI HII Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top