728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, October 16, 2015

    NASEPA:LUIS ENRIQUE KUITEMA BARCA MWISHO WA MSIMU


    Kocha wa FC Barcelona Luis Enrique amesema kuwa ataachana na klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu ikiwa atapata nafasi ya kuinoa timu ya taifa ya Hispania inayonolewa na Vicente del Bosque kwa sasa.

    Enrique,41 ameyasema hayo leo ijumaa wakati wakiongelea masuala mbalimbali ya soka ikiwemo michezo ya klabu yake hasa La Liga na Uefa.Kauli hiyo ya Enrique imedaiwa kuiweka njia panda FC Barcelona kwani italazimika kutafuta kocha mwingine ikiwa jambo hilo litafanikiwa.Enrique ambaye januari ya mwaka huu aliingia katika mgogoro mkubwa na wachezaji nyota wa klabu hiyo ameonyesha hamu kubwa ya kuifundisha Hispania aliyowahi kuichezea michezo 62 ndani ya kipindi cha miaka 11baada ya kukiri waziwazi kuitaka nafasi hiyo.Inaaminika kuifundisha Hispania hakuna presha kama kuifundisha FC Barcelona.

    Barcelona's players throw Barcelona's coach Luis Enrique in the air

    Vicente del Bosque anatarajiwa kuachia ngazi kuifundisha Hispania baada ya michuano ijayo ya Ulaya itakayofanyika mwaka 2016 huko Ufaransa na tayari kocha wa Rayo Vallecano Paco Jemez ameanza kutajwa kuwa mrithi wa kocha huyo wa zamani wa Real Madrid.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: NASEPA:LUIS ENRIQUE KUITEMA BARCA MWISHO WA MSIMU Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top