Glasgow, Scotland.
Mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Chelsea na Westham Carlton Cole leo amesaini mkataba wa miaka miwili kuwachezea mabingwa wa Scotland klabu ya Celtic akiwa kama mchezaji huru baada ya kutemwa na Westham msimu uliopita.
Cole,32 amesaini mkataba huo utakaoisha 2017 baada ya kufaulu majaribio aliyoyafanya klabu hapo kwa siku kadhaa na mchezo wake wa kwanza utakuwa wikendi hii ambapo Celtic itakapovaana na timu iliyomkiani ya Dundee United lakini hataweza kuichezea Celtic kwenye michuano ya Europa Ligi kwa kuwa usajili kwa ajili ya michuano hiyo ulishafungwa kitambo.
Cole alifanikiwa kuichezea Westham michezo 250 na kuifungia zaidi ya magoli 50 licha ya kukumbwa na majeruhi ya mara kwa mara.
0 comments:
Post a Comment