728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, October 20, 2015

    CANNAVARO AWACHAMBUA MKWASSA,MWAMBUSI


     
    NAHODHA wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amemchambua kocha mpya msaidizi wa timu hiyo, Juma Mwambusi na kumlinganisha na aliyekuwa kocha msaidizi wa klabu hiyo, Charles Boniface Mkwasa na kusema wawili hao hawana tofauti kabisa.

    Mwambusi alichukua mikoba ya Mkwasa ya kuwa msaidizi wa kocha, Hans Van Pluijm wiki iliyopita baada ya Mkwasa kupewa mkataba wa mwaka mmoja na nusu wa kuinoa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

    Akizungumza na BINGWA, Cannavaro alisema kuwa katika kipindi alichokaa na Mwambusi amegundua kuwa kocha huyu hapendi utani kwenye suala zima la nidhamu za wachezaji na siku zote amekuwa akisisitizia suala hilo kama ilivyokuwa kwa Mkwasa.

    Cannavaro alisema kuwa kutokana na hali hiyo, hivi sasa ana matumaini makubwa sana na timu yao na nidhamu haitakuwa tatizo kwenye kikosi cha Yanga kitu ambacho kitachangia kuwapa ubingwa mapema msimu huu.

    “Kwa muda mfupi niliokuwa na Mwambusi baada ya kurejea kutoka Stars nimeona anaweka mbele masuala ya nidhamu na kujituma kuliko kitu chochote na hivi ndivyo alivyokuwa Mkwasa,” alisema Mwambusi.

    “Mwambusi ni mtu wa utani sana na tabia yake hii imesababisha wachezaji tumzoee haraka sana na tunaona kama tumekaa naye zaidi ya mwaka, kinachonifurahisha zaidi ni kuwa anapita kwenye njia zile zile za Mkwasa, hii itatusaidia kutupa matokeo bora na inafahamika kuwa ili timu iwe bora lazima nidhamu izingatiwe,” alisema Cannavaro.

    Cannavaro aliwataka pia wachezaji wa kikosi hicho kufanya kazi kiweledi, kujituma na kufuata kila wanaloelekezwa na benchi la ufundi kwani bado wana safari ndefu yenye changamoto kuelekea katika kutetea ubingwa wao.
     
    (Chanzo:Gazeti la Bingwa)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: CANNAVARO AWACHAMBUA MKWASSA,MWAMBUSI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top