728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, October 18, 2015

    MABADILIKO:MANCHESTER CITY YAJIPANGA KUIPIGA BAO ARSENAL

    Manchester,England.

    Mambo yakienda kama yalivyopangwa basi Manchester City itakuwa imeipiku Arsenal kwa kuwa na uwanja unaochukua watazamaji wengi zaidi.

    Kutoka jiji la Manchester habari zinasema Manchester City inapanga kuupanua uwanja wake wa Etihad kutoka kuchukua watazamaji 54,000 mpaka watazamaji 61,000.

    Kazi hiyo ya upanuzi inatarajiwa kufanyika mwishoni mwa msimu huu na endapo mipango itafanikiwa basi uwanja wa Etihad utakuwa umechukua nafasi ya pili kwa ukubwa na kuuzidi uwanja wa Emirates unaomilikiwa na Arsenal wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000.

    Kwa sasa uwanja wa Old Trafford unaomilikiwa na Manchester United ndiyo unaongoza kwa kuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 76,000 ukifuatiwa na Emirates wenye 60,000 na kisha Etihad wenye watazamaji 54,000.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MABADILIKO:MANCHESTER CITY YAJIPANGA KUIPIGA BAO ARSENAL Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top