Muitaliano Carlo Ancelotti ndiye atakayerithi mikoba ya Pep Guardiola katika klabu ya Bayern Munich msimu ujao hii ni kwa mujibu wa mtandao wa Sport Mediaset wa Italia.
Sport Mediaset imeongeza kuwa Ancelotti na Bayern Munich tayari wameshafanya makubaliano ya awali na kocha huyo wa zamani wa vilabu vya AC Milan,Chelsea,PSG na Real Madrid amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili ili kuziba nafasi ya Guardiola anayesemekana kutimkia Manchester City pindi mkataba wake utakapoisha mwishoni mwa msimu huu.
Ancelotti ambaye alikuwa akifukuziwa na klabu ya Liverpool ili kuchukua nafasi ya Brendan Rodgers kabla ya kudengua amekuwa hana timu tangu alipotimuliwa na Real Madrid msimu uliopita.
0 comments:
Post a Comment