London,England.
HATARI:Mshambuliaji wa Arsenal Mfaransa Olivier Giroud ndiye mchezaji aliyefunga magoli mengi zaidi kwa kutumia kichwa chake katika ligi kuu England baada ya kufunga magoli 14 tangu atue katika ligi hiyo msimu wa 2012/2013.
Giroud,29 alijiunga na Arsenal msimu wa 2012/2013 akitokea Montpellier ya nyumbani kwao Ufaransa kwa ada ya paundi milioni 12 alifikisha idadi hiyo ya magoli baada ya kuifungia Arsenal goli la kuongoza kwa kichwa wikendi iliyopita katika mchezo ambao Arsenal iliibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Everton.
Mbali ya Giroud,mshambuliaji wa Liverpool Mbelgiji Christian Benteke naye amefunga idadi hiyo hiyo ya magoli tangu atue England msimu wa 2012/2013 akitokea Gent ya nyumbani kwao Ubelgiji.Goli la kichwa alilofunga Benteke wikendi iliyopita dhidi ya Southampton limemfanya afikishe magoli 14.
Hii hapa orodha ya wakali wa magoli ya vichwa tangu 2012/2013
Olivier Giroud – 14
Christian Benteke – 14
Romelu Lukaku – 10
Peter Crouch – 10
.
0 comments:
Post a Comment