London,England.
Arsenal imepata pigo baada ya nyota wake wawili Aaron Ramsey na David Ospina kutarajiwa kuwa nje ya dimba kwa kipindi cha mwezi mmoja kila mmoja baada ya kupata majeruhi.
Ramsey atakuwa nje kwa jeraha la misuli lililomlazimu kutolewa uwanjani dakika ya 57 wakati akiichezea Arsenal katika mchezo wa jumanne wa ligi ya mabingwa wa Ulaya dhidi ya Bayern Munich.
Kufuatia jeraha hilo Ramsey ataukosa mchezo wa ligi kuu jumamosi hii dhidi ya Everton kisha mchezo wa Novemba 8 dhidi ya Tottenham Hotspur na mchezo wa Novemba 13 ambapo timu yake ya taifa ya Wales itakuwa ikivaana na Uholanzi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.
David Ospina yeye bado anasumbuliwa na jeraha alilolipata wakati akiitumikia Colombia katika kinyang'anyiro cha kusaka tiketi ya kusaka kombe la dunia 2018 nchini Urusi.
0 comments:
Post a Comment