Munich,Ujerumani.
Meneja wa Bayern Munich Muhispania Pep Guardiola ameonyesha mahaba mazito kwa nyota wake David Alaba na kusisitiza nyota huyo mwenye miaka 23 ni Mungu wa kikosi hicho kwasababu amecheza katika nafasi zote za ndani uwanjani isipokuwa nafasi ya golikipa tu.
Akifanya mahojiano na kituo cha Sport kuelekea mchezo wa leo jumamosi wa ligi ya Bundesliga dhidi ya FC Koln,Guardiola amesifu uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani alionao David Alaba nyota toka Austria na kusema
“David Alaba ni kama Mungu wetu. Amecheza karibu nafasi zote 10 uwanjani.Ni mchezaji wa kipekee sana”Alisema Guardiola.
Alaba alijiunga na Bayern mwaka 2008 wakati huo miamba hiyo ya Bundesliga ikiwa chini ya Louis Van Gaal kisha Jupp Hynenkess na chini ya Guardiola,Alaba amekuwa mmoja kati ya nyota waliokamilika zaidi duniani.
Tangu ujio wa Guardiola tayari Alaba ameshacheza katika nafasi ya ulinzi wa kushoto,kiungo mkabaji,mlinzi wa kati na nafasi nyingine kadha wa kadha.
0 comments:
Post a Comment