Istanbul,Uturuki.
BEKI wa kimataifa wa Ureno, Képler Laveran Lima Ferreira maarufu kama Pepe sasa atajiunga na miamba wa soka wa nchini Uturuki,Besiktas mara baada ya mkataba wake na Real Madrid kufikia mwisho.
Hivi karibuni beki huyo mwenye umri wa miaka 34 aliripotiwa kuwa mbioni kujiunga na miamba wa soka nchini Ufaransa Paris Saint-Germain lakini mpango huo ulikwama katika dakika za mwisho.
Kwa mujibu wa mtandao wa Macca,taarifa zinasema Pepe anayesifika kwa kucheza soka la kibabe tayari alishafanyiwa mpaka vipimo vya afya na klabu hiyo ya jiji la Paris lakini madai yake makubwa ya mshahara yalifanya uhamisho huo ufe.
Sasa taarifa zinasema tayari wawakilishi wa Pepe wameshafikia makubaliano na Besiktas na kinachosubiriwa kwa sasa ni beki huyo kwenda kumwaga wino wa kuichezea klabu hiyo.
0 comments:
Post a Comment