Rustenburg, Afrika Kusini.
KOCHA MKUU wa Bafana Bafana,Stuart Baxter ameamua kuanzisha wachezaji wanane wapya kwenye kikosi chake cha kwanza ambacho leo jioni kitashuka dimbani huko Royal Bafokeng kucheza na Tanzania katika mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu nusu fainali ya michuano ya kombe la Cosafa Castle.
Mlinda mlango Boalefa Pule leo atakuwa anaichezea Bafana Bafana mchezo wake wa kwanza.Wengine ni mabeki wa kulia,kushoto na kati Thendo Mukumela,Innocent Maela na Mario Booysen ambao wataungana na Lorenzo Gordinho ambaye mpaka sasa ameshaichezea Bafana Bafana mchezo mmoja.
Nahodha Lehlogonolo Masalesa na yeye atakuwa anavaa jezi ya Bafana Bafana kwa mara ya kwanza.Atacheza nafasi ya kiungo cha ulinzi akisaidiwa na mzoefu Cole Alexander aliyeongezwa kikosini kuchukua nafasi ya Aubrey
Ngoma aliyeumia goti.
Winga wa Orlando Pirates,Riyaad Norodien atakuwa anacheza mchezo wake wa kwanza akiwa na Bafana Bafana kama ilivyo kwa winga Liam Jordan na kiungo Jamie Webber.
Kikosi kamili cha Bafana Bafana kiko kama ifuatavyo:(GK), Thendo Mukumela, Innocent Maela,Lorenzo Gordinho,Mario Booysen,Lehlogonolo Masalesa (C), Cole Alexander,Riyaad Norodien, Jamie Webber, Liam Jordan,Judas Moseamedi.
Tanzania: Aishi Manula,Shomari Kapombe,Gadiel Michael,Salim Mbonde,Erasto Nyoni,Himid Mao,Thomasi Ulimwengu,Mzamiru Yassin,Elias Maguli,Raphael Daud na Shiza Kichuya
0 comments:
Post a Comment