728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, July 01, 2017

    MZIMBABWE AMPIGA GEPU SHIZA KICHUYA UFUNGAJI BORA COSAFA

    Ovidy Obvious Karuru mwenye mpira


    Rustenburg, Afrika Kusini.

    MAJAALIWA ya winga wa Tanzania,Shiza Ramadhan Kichuya kuibuka mfungaji bora wa michuano ya kombe la Cosafa Castle inayoendelea huko nchini Afrika Kusini yameanza kupotea baada ya mpinzani wake wa karibu Mzimbabwe,Ovidy Obvious Karuru kuendelea kufumania nyavu bila kuchoka.

    Karuru anayeichezea AmaZulu inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Afrika Kusini jana Ijumaa aliifungia Zimbabwe mabao matatu katika ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Ushelisheli na hivyo kufikisha mabao matano katika michezo mitatu.

    Ikumbukwe katika mchezo wa kwanza wa kundi B,Karuru ambaye ni nahodha wa Zimbabwe kwenye michuano ya mwaka huu alifunga mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Msumbiji.

    Mabao hayo mawili yalimfanya Karuru,28,awe sawa na Kichuya aliyekuwa ameifungia Tanzania,Taifa Stars mabao mawili kwenye mchezo wake wa ufunguzi wa kundi A dhidi ya Malawi.

    Lakini kushindwa kufunga mabao kwa Kichuya katika michezo miwili iliyopita dhidi ya Angola na Mauritius kumetoa mwanya kwa Karuru aliyewahi kukipiga Ufaransa na Ubelgiji kujiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kuwa mfungaji bora wa michuano ya mwaka huu ya Cosafa Castle.

    Ili kufufua matumaini kutwaa kiatu cha ufungaji bora,Kichuya sasa anapaswa kuifungia Taifa Stars mabao zaidi ya matatu kwenye mchezo wake wa robo fainali dhidi ya wenyeji Afrika Kusini.

    Mchezo kati ya Taifa Stars na Afrika Kusini utachezwa kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace kuanzia Saa 12:00 jioni.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MZIMBABWE AMPIGA GEPU SHIZA KICHUYA UFUNGAJI BORA COSAFA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top