Rustenburg, Afrika Kusini.
TIMU ya taifa ya Tanzania,Taifa Stars kwa mara ya kwanza leo imefanikiwa kufuzu hatua ya nusu ya fainali ya michuano ya kombe la Cosafa Castle baada ya jioni ya leo kuwafunga wenyeji na mabingwa watetezi wa michuano hiyo Afrika Kusini kwa jumla ya bao 1-0 katika mchezo wa robo fainali uliochezwa huko Royal Bafokeng,Rustenburg, Afrika Kusini.
Bao lililoipa ushindi Taifa Stars siku hii ya leo limefungwa katika dakika ya 18 kwa mkwaju mkali wa mbali na Elias Maguri baada ya kupokea pasi ndefu ya Muzamiru Yassin.
Ushindi huo licha ya kuipeleka Taifa Stars nusu fainali ya Cosafa Castle kwa mara ya kwanza katika historia bali umefuta uteja wa muda mrefu wa kufungwa mara mbili na Afrika Kusini mwaka 2002 na 2011.
Vikosi:Bafana: Pule (GK), Mukumela, Maela,Gordinho, Booysen, Masalesa (c),Alexander,Norodien (Maboe 77'),Webber,Jordan (Mokate 60'),Moseamedi.
Tanzania: Manula, Kamagi, Nyoni, Mbonde,Mao, Maguri, Ulimwengu, Loth, Ramadhani,Said, Kapombe.
0 comments:
Post a Comment