728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, July 02, 2017

    REKODI MBAYA DHIDI YA BAFANA BAFANA ZAICHONGEA TAIFA STARS


    Rusternburg,Afrika Kusini.

    TIMU ya taifa ya soka ya Tanzania,Taifa Stars leo jioni mishale ya saa 12:00 za jioni itashuka kwenye Uwanja wa Royal Bafokeng ulioko karibu na mji wa Rustenburg kucheza mchezo wake wa robo fainali wa michuano ya kombe la COSAFA Castle kwa kuvaana na mabingwa watetezi ambapo pia ni wenyeji Afrika Kusini,Bafana Bafana.

    Taifa Stars inayonolewa na mzawa,Salum Mayanga inaingia kwenye mchezo wa leo ikiwa na rekodi mbili mbaya za kushindwa kupata ushindi wowote dhidi ya miamba hao wa kusini mwa bara la Afrika.

    Ikumbukwe kabla ya mchezo wa leo, Taifa Stars imeshawahi kukutana na Bafana Bafana mara mbili katika nyakati tofauti na katika mara hizo zote imeshindwa kupata matokeo ya ushindi.

    Mara ya kwanza timu hizo zilikutana mwaka 2002 kwenye michuano ya Cosafa Castle iliyoshirikisha timu nne pekee,Bafana Bafana iliitupa nje Taifa Stars kwa penati 4-3 baada ya sare ya kufungana bao 1-1 katika muda wa kawaida.

    Mara ya pili timu hizo zilikutana mwaka 2011 kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam na Bafana Bafana ilishinda kwa bao 1-0 lililofungwa na Siyabonga Sangweni.

    Rekodi hizo mbili zinainyia Taifa Stars nafasi ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa leo huku ikizingatiwa kuwa inakutana na Bafana Bafana itakayokuwa inacheza kwenye uwanja wake wa nyumbani huku pia ikitaka kuutetea ubingwa wake iliyoutwaa mwaka jana kwa kuifunga Botswana mabao 3-2 kwenye mchezo wa fainali uliochezwa huko Windhoek,Namibia.

    Mshindi kati ya Taifa Stars na Bafana Bafana katika mchezo wa leo atafuzu nusu fainali na kuvaana na mshindi kati ya Botswana na Zambia siku ya Jumatano Julai 5.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: REKODI MBAYA DHIDI YA BAFANA BAFANA ZAICHONGEA TAIFA STARS Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top