728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, July 04, 2017

    EVERTON YAZIDI KUKIONGEZEA SUMU KIKOSI CHAKE,YAMNASA KEANE WA BURNLEY


    Liverpool, England.

    ILI kuhakikisha kuwa inakuwa na kikosi kipana,kikali na chenye uwezo wa kufanya lolote msimu ujao, Everton imeendelea kukiongezea sumu kikosi chake hii ni baada ya usiku wa kuamkia leo kumsajili beki wa kati wa kimataifa wa England,Michael Keane kutoka Burnley kwa mkataba wa miaka mitano.

    Keane mwenye umri wa miaka 24 amejiunga na Everton kwa ada ya uhamisho ambayo itapanda na kufikia rekodi ya klabu ya £30m ambayo kwa sasa inashikiliwa na mlinda mlango,Jordan Pickford aliyetua klabuni hapo mwezi uliopita akitokea Sunderland.

    Akifanya mahojiano baada ya kukamilisha taratibu zote za uhamisho wake,Keane amesema amejiunga na Everton kwa kuwa ameona ni sehemu sahihi kwake na kuongeza kuwa kocha wa klabu hiyo Mdachi,Ronald Koeman ndiye aliyemvutia hata akakubali kumwaga wino klabuni hapo kwa kuwa na yeye alikuwa akicheza nafasi ya beki wa kati kama yeye.

    Keane aliyejiunga na Burnley Januari 2015 akitokea Manchester United kwa ada ya uhamisho £2m anaamini kuwa karibu na Koeman kutamfanya ajifunze mambo mengi yatakayomfanya awe mwiba mchungu zaidi kwa washambuliaji wasumbufu.

    Keane anakuwa mchezaji wa tano kujiunga na Everton katika kipindi cha usajili barani Ulaya.Wengine ni Jordan Pickford,Davy Klaassen,Henry Onyekuru na Sandro Ramirez.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: EVERTON YAZIDI KUKIONGEZEA SUMU KIKOSI CHAKE,YAMNASA KEANE WA BURNLEY Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top