Dar Es Saam,Tanzania.
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake Selestine Mwesigwa wamenyimwa dhamana na hivyo wamerudishwa rumande ambapo Kesi yao itatajwa tena Julai 17 mwaka huu.
Leo Jumatatu Malinzi na wenzie walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kufuatia kushtakiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa makosa 28 yakiwemo ya utakatishaji fedha.
0 comments:
Post a Comment