728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, July 03, 2017

    LUKAS PODOLSKI AJIUNGA NA KOBE



    Tokyo, Japan.

    NYOTA wa zamani wa Arsenal,Bayern Munich na timu ya taifa ya Ujerumani,Lukas Podolski ameihama Galatasaray na kujiunga na Vissel Kobe ya ligi kuu nchini Japan maarufu kama J-League.

    Podolski mwenye umri wa miaka 32 ametumia ukurasa wake wa twitter kuthibitisha uhamisho huo kwa kuweka picha inayomwonyesha akiwa amevalia jezi No.10 ya timu yake hiyo mpya na ujumbe usemao 'The beginning of my next chapter.' (Mwanzo Wa Ukurasa Wangu Mpya).

    Podolski ameihama Galatasaray baada ya kuitumikia kwa misimu miwili akitokea Arsenal.

    Vissel Kobe inayotumia uwanja wa Noevir kwa michezo yake ya nyumbani inashika nafasi ya 11 kwenye ligi kuu soka ya nchini Japan yenye timu 18.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: LUKAS PODOLSKI AJIUNGA NA KOBE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top