Dar Es Salaam,Tanzania.
KATIKA hali isiyotarajiwa mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa kuwapata viongozi wapya wa Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) uliokuwa ukiendelea umetangazwa kusitishwa kwa muda hadi hapo utakapotangazwa tena.
Maamuzi hayo yametangazwa leo na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Wakili Rovocatus Kuuli katika mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika kwenye ofisi za TFF zilizoko Karume jijini Dar Es Salaam.
Kuuli amesema hilo limefikiwa baada ya yeye kama mwenyekiti kutofautiana na wajumbe wa kamati yake siku ya jana juu ya wagombea ambao wanashikiliwa na vyombo dola kama wana haki ya kupitishwa ama kutopitishwa licha ya kutokuwepo kwenye usaili ulioanza tangu juzi.
Wagombea waliokosa kufanyiwa usaili kutoka na kushikiliwa na vyombo dola ni Jamal Malinzi ambaye ni Rais wa sasa wa TFF pamoja na makamu wake wa pili Geoffrey Nyange Kaburu ambao wako rumande kwa tuhumu mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka.
0 comments:
Post a Comment