Brisbane,Australia.
BONDIA wa Ufilipino,Manny Pacquiao ameendelea kuonyesha dalili za kutorejea tena kwenye makali yake ya zamani hii ni baada ya leo asubuhi kudundwa na bondia asiye na jina kubwa Jeff Horn wa Australia katika pambano la kugombea mkanda wa WBO la raundi 12 lililofanyika kwenye Uwanja wa Suncorp huko Brisbane,Australia na kushuhudiwa na watazamaji 50,000.
Jeff Horn,27,ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi Pallara State School amebuka mshindi dhidi ya Pacquiao,38 baada ya majaji kumpa ushindi wa pointi 117-111, 115-113 na 115-113.
Ushindi huo umemfanya Jeff Horn kuweka rekodi ya kushinda mapambano 17 na kutoka sare pambano 1 kati ya mapambano 18 aliyoyacheza mpaka sasa.
Wakati huohuo Jeff Horn amejinyakulia kitita cha Dola 500,000 ambacho ni sawa na Shilingi Bilioni 1.2 kama zawadi ya kumchapa Pacquiao mwenye rekodi ya kushinda mapambano 58.
0 comments:
Post a Comment