728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, July 03, 2017

    RASMI:JOHN TERRY ATUA ASTON VILLA


    Birmingham,England.

    KLABU ya Aston Villa inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini England maarufu kama Championship imetangaza kumsajili beki wa zamani wa Chelsea na England,John Terry kwa mkataba wa mwaka mmoja.

    Terry mwenye umri wa miaka 36 sasa amejiunga na Aston Villa akiwa mchezaji huru mara baada ya Chelsea kuamua kutompa mkataba mpya.

    Terry anaiacha Chelsea baada ya kuhudumu kwa kipindi cha miaka 20 akiwa ameichezea zaidi ya michezo 717 akitwaa mataji makubwa 15 yakiwemo mataji matano ya ligi kuu ya soka nchini England.

    Taarifa zaidi zinasema Terry atakuwa akilipwa mshahara wa £60,000 kwa wiki na atajipatia kitita cha £4m ikiwa ataisaidia klabu kurejea ligi kuu.

    Mbali ya kitita hicho cha fedha pia Aston Villa imemuahidi Terry kumjumuisha kwenye benchi lake la ufundi pindi atakapomaliza mkataba wake klabuni hapo.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: RASMI:JOHN TERRY ATUA ASTON VILLA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top