Roma,Italia.
AS ROMA imefanikiwa kumrejesha nyumbani kwa mara nyingine kiungo wake wa zamani,Lorenzo Pellegrini aliyekuwa akiichezea klabu ya Sassuolo.
Pellegrini mwenye umri wa miaka 21 amerejea AS Roma kwa dau la €10m ikiwa ni misimu miwili imepita tangu aihame klabu hiyo mwaka 2015 kwa dau la €1.5m.
Kiungo huyo mzaliwa wa Italia amejiunga na AS Roma kwa mkataba wa miaka mitano utakaodumu mpaka 2022 na atakuwa akivalia jezi No.7 ambayo msimu uliopita ilikuwa ikivaliwa na Mfaransa, Clement Grenier aliyerejea Lyon baada ya uhamisho wake wa mkopo kuisha.
Katika misimu miwili aliyokuwa na Sassuolo, Pellegrini alifanikiwa kucheza michezo 54.Msimu uliopita alicheza michezo 28 na kufanikiwa kufunga mabao sita huku akipika mengine saba.
0 comments:
Post a Comment