Magoli mawili ya kiungo Juan Mata na mlinzi Chris Smalling yameipa ushindi Manchester United wa goli 2-1 dhidi ya Wolfsburg katika mchezo mkali wa kundi B wa ligi ya mabingwa Ulaya uliopigwa katika dimba la Old Trafford jumatano usiku.
Manchester United ilibidi ipigane kiume ili kuibuka na ushindi huo kwani ilijikuta ikiwa nyuma kwa goli la mapema la dakika ya 4 la Daniel Caligiuri.Kuingia kwa goli hilo kuliiamsha Manchester United na hatimaye kupata magoli yake dakika za 34 kupitia kwa Juan Mata aliyefunga kwa penati baada ya kufanyiwa madhambi katika eneo la hatari huku lile la pili likifungwa na Chris Smalling akimalizia vyema pasi ya Juan Mata.
Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo Manchester City iliyo kundi D nayo imeibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Borussia Moenchengladbach shukrani kwa magoli ya Nikolas Otamendi na Sergio Aguero huku lile la Moenchengladbach ilifungwa na Lars Stindl.
Matokeo mengine ya ligi ya mabingwa
Malmo FF 0-2 Real Madrid
Shaktar Donestik 0-3 PSG
Juventus 2-0 Sevilla
Astana 2-2 Galatasaray
Atletico Madrid 1-2 Benfica
CSKA Moscow 3-2 PSV Eindhoven
0 comments:
Post a Comment