Mexico City,Mexico.
SHIRIKISHO la Soka Ulimwenguni FIFA limemteua Mwanamama Fatma Samba Diouf Samoura toka Senegal kuwa Katibu wake Mkuu Mpya.
Akitangaza uteuzi huo Rais wa Shirikisho hilo Gianni Infantino amemuita Fatuma,54 kuwa ni Mwanamama Jasiri na Mchapakazi mwenye Uzoefu wa kufanya Kazi katika mashirika ya Kimataifa.
Fatuma mwenye uwezo wa kuongea kwa ufasaha lugha za Kifaransa,Kiingereza,Kihispania na Kiitalia na mwenye uzoefu wa miaka 21 wa kufanya kazi katika mashirika ya Kimataifa anakuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo mkubwa FIFA.Ataanza Kazi yake hiyo mpya mwezi Juni.
Tayari Fatuma ameshafanya kazi za Uwakilishi na Ukurugenzi katika mataifa sita ya Djibouti, Cameroon,Chad, Guinea, Madagascar na Nigeria anayohudumu mpaka sasa.
Wakati huohuo FIFA imeyaongeza katika orodha ya wanachama wake wapya mataifa ya Kosovo na Gibraltar na kufikisha idadi ya wanachama 211.
Kwa maana hiyo Kosovo na Gibraltar zimepata haki ya kuingia katika kinyang'anyiro cha kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya kombe la dunia la mwaka 2018 huko Urusi.
0 comments:
Post a Comment